Mdomo Uliponza Kichwa Lyrics

Lyrics & meaning

Mdomo Uliponza Kichwa

Soul Touch Brand

ReleasedMarch 9, 2026 GenreAfro-Beat

About this song

Mdomo Uliponza Kichwa Lyrics

Mdomo Uliponza Kichwa is a captivating Swahili Afro-Beat masterpiece, brought to life by the artistic prowess of Soul Touch Brand. The song’s lyrics and music are the handiwork of Giveness Alfred Ngao, demonstrating expertise in both composition and production, capturing the essence of this creation through versatile talent. Mdomo Uliponza Kichwa was released on March 9, 2026. “Mdomo Uliponza Kichwa Lyrics” has stayed with many, making it a song people naturally come back to again and again. Below, you’ll find the lyrics for Soul Touch Brand’s “Mdomo Uliponza Kichwa”, offering a glimpse into the profound artistry behind the song.

Listen to the complete track on Amazon Music

Choose your script

Read the Song Lyrics

Lyrics text size: 100%

Mdomo uliponza kichwa
Chunga sana kinywa chako
Usinene mabaya, usinene mabaya
Baraka, upate baraka

Leo unaongea juu yangu
Kesho yatakuzunguka wewe
Ukimtupa mwenzio kwenye kivuli
Kesho mwanga utakukosa tena

Ukicheka machozi ya jirani (JE,)
Ukilia nani atabaki
Kile unachokisema kwa hasira
Kina rudi moyoni
Kina kuunguza pole pole

Wewe sema wema (ukisema)
Sema kwa upendo
Wewe kata tamaa ya Laana
Ukimwaga uchungu
Utakunywa mwenyewe

(Mdomo uliponza kichwa)
Chunga sana kinywa chako
(Usinene mabaya), usinene mabaya
(Baraka, upate baraka)
Baraka (baraka), baraka

Ukitamka heri (Heri)
Heriitarudi (huuuu)
Ukitupa Moto (Moto)
Moto utakuchoma

(Mdomo uliponza kichwa)
Chunga sana kinywa chako

Ulisema hatafanikiwa (Sasa)
Unaangalia kwa wivu
Maneno Yako yanakufunga miguu
Unabaki palepale

Unaumia kimya kimya
Ukimdharau aliye chini
Utakutana nae juu ya ngazi
Ukitila uchungu kwenye damu
Utasahau ladha ya amani moyoni

Wewe sema wema (ukisema)
Sema kwa upendo
Usiweke sumu kwenye ndimi
Ukiwasha vita
Vita vitabaki kwako

(Mdomo uliponza kichwa)
Chunga sana kinywa chako
(Usinene mabaya), usinene mabaya
(Baraka, upate baraka)
Baraka (baraka), baraka

Ukitamka heri (Heri)
Heriitarudi (huuuu)
Ukitupa Moto (Moto)
Moto utakuchoma

(Mdomo uliponza kichwa)
Chunga sana kinywa chako, hey!

Hey, kwa kila neno
Kuna mbegu inachipuka
Utapanda Nini leo
Kesho utakuta shamba lako

Kwa Kila laana
Kuna mlango unafungwa
Ukibariki wengine
Baraka zako zinaongezeka

(Mdomo uliponza kichwa)
Chunga sana kinywa chako
(Usinene mabaya), usinene mabaya
(Baraka, upate baraka)
Baraka (baraka), baraka

Ukitamka heri (Heri)
Heriitarudi (huuuu)
Ukitupa Moto (Moto)
Moto utakuchoma

(Mdomo uliponza kichwa)
(Baraka, upate baraka)
Chunga sana kinywa chako
(Usinene mabaya, usinene mabaya)
Chunga sana (kinywa chako)

Oh, yeah!